Katibu tawala wilayani Kalambo mkoani Rukwa Servi Ndumbalo amewataka walimu kushirikina watendaji wa serikali za vijjiji katika kudhibiti vitendo vya utoro kwa wanafunzi kwa kutoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya umuhimu wa watoto kupata elimu.
Aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa elimu wilayani humo na kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Kalambo na kusisitiza watendaji wa serikali za vijiji na kata kushirikana na walimu katika kudhibiti vitendo vya utoro kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kuongeza ufaulu.
Aidha aliwataka viongozi wa serikali kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kujiepusha na vitendo viovu ambavyo vinaweza kusababisha taharuki katika jamii na kusisistiza viongozi kuwa mfano katika kauli na matendo ili kuwezesha waliochini kuishi matendo yao.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Sandy Wambula aliwataka watumishi kufanya kazi kwa weredi ili kufikia malengo ya serikali.
Baadhi ya walimu wilayani humo walisema wamejipanga kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kwa kufanya kazi kwa weredi kwa kuhakikisha wanafunzi wote wanahudhuria vipindi madarasani.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.