Imeelezwa kuwa uchaguzi huru na wa haki ndiyo nyenzo kuu ya sasa kwaa jili ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda, na kwamba lengo hilo haliwezi kufikiwa endapo Watanzania wenyewe watashindwa kuchagua viongozi wazalendo,hodari na waadilifu wasiobagua watu kwa misingi ya dini, rangi na itikadi za kisiasa.
Akiwa katika ziara ya ukaguzi wa vituo vya kuandikisha wapiga kura katika kata za Mpombwe, Kisumba na Katete ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika 24 Novemba 2019, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura amewataka maafisa waandikishaji, mawakala na wananchi wote kuhakikisha wanaitendea haki nchi kwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuwabaini raia wa kigeni wasishiriki uchaguzi huo.
Amesema Mawakala wa vyama vya siasa wanalojukumu la kuwasaidia waandikishaji kuwatambua wageni ili wasijiandikishe kwenye daftali la wapiga kura kwani hawana haki hiyo na kwamba wakimtilia shaka mtu yeyote watumie mbinu mbadala za uchunguzi zikiwemo Kiswahili anachoongea,
‘’ tumieni njia mbadara kuwatambua wageni wanao toka nchi jilani kwa kuwataka kuimba wimbo wa Taifa la Tanzania pia mawakala wa vyama vya siasa kuweni makini na msichukue majina ya wapiga kura wanaoandikishwa lengo likiwa ni kuepuka kutawanya nyaraka hizo suala ambalo litapelekea kubatilisha uchaguzi hapo baadaye’’alisisitiza Binyura.
Naye Kamanda wa TAKUKURU Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa Lupakisyo Mwakyolile amewataaka wananchi kutoa taarifa kwenye vyombo husika pindi kunapotokea viaashiria vya rushwa kwenye maeneo yao husika.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.