Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura amewagiza maafisa elimu wa shule za msingi na sekondari wilayani humo kuanzisha mashaba darasa ya kilimo na kuhakikisha wanafunzi wote wanapata chakula cha mchana ikiwa ni jitihada za kutokomeza hali ya udumavu ambayo katika mkoa ni asilimia 47.9.
akiongea na kamati za lishe wilayani humo mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura ,amesema lengo la serikali ni kuhakikisha hali ya udumavu na utapiamlo hususani kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano unatokomea.
‘’tatizo la udumavu na utapia mlo ni tatizo linalo athiri ukuwaji ubongo na afya ya watoto,takwimu za kitaifa zinaonesha mkoa wa Rukwa unaongoza kwa tatizo la udumavu na utapia mlo hii inajumuisha Halmashauri ya Kalambo, katika kukabiliana na tatizo hili, idara zote ni muhimu zikashirikiana kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kula vyakula bora.’’alisema Binyura.
Alisema kwa ujumla lishe duni na ulaji wa vyakula vya aina moja ni miongoni mwa sababu zinazo sababisha udumavu na utapia mlo kwa watoto.
‘’Ili jamii iweze kuondokana na tatizo la udumavu na utapia mlo ni lazima ihamasishwe kwa kuzingatia mpangilio sahihi wa lishe bora ikiwa ni pamoja na kuepuka ulaji wa vyakula vya aina moja ‘’alisema Binyura.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Nicholaus Mlango, amesema kwa mwaka 2019/2020 Halmashauri imefanikiwa kutenga fedha kiasi cha shilingi milioni 60 ikiwa ni utekelezaji wa agizo la waziri wa nchi ofisi ya rais tamisemi la kutenga fedha kiasi cha shilingi elfumoja kwa kila mtoto mwenye hali ya udumavu.
‘’elimu ya uzalishaji wa mbogamboga na matunda kama beetroot{viazi vyekundu ,viazi lishe,butter nut ,tango,na mahindi ya njano ni muhimu wananchi wakahamasishwa kuvilima kwa ajili ya manufaa yao ‘’alisema Mlango.
Afisa elimu msingi wilayani humo Rose Mganga ,amesema kwa kutambua umuhimu wa swala hilo wameanzisha mashamba darasa ya matunda na mbogamboga katika shule za msingi na sekondari.
‘’tumeanzisha mashamba ya matunda ya Mapapai na mbogamboga ,ambazo ni mchicha na chines ,na pia tunalima shamba la alizeti ,hivyo tunakamua mafuta yanayotumika kwa kupikia ‘’alisema Mganga.
Dani Hinjo kutoka shirika lisilo la kiserikali la advancent for sustainable community {ASCO}amesema wanaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa lishe hususani kwa akina mama wajawazito na makundi ya vijana.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.