mkuu wa wilaya kalambo mkoani rukwa, Julieth Binyura ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kuchunguza kwa umakini tuhuma za makosa ya ukatili wa kijinsia na mila potofu ili kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii.
Binyura alitoaa agizo hilo wakati wa utambulisho wa mradi wa kupinga mila potofu na ukatili wa kijinsia-sucoda- wilayani kalambo ambapo alisema vitendo hivyo vinakwamisha juhudi za wananchi kushirikiki kikamilifu katika shughuli za maendeleo
Alisema makosa ya ukatili wa kijinsia yanachangia kwa kiasi kikubwa kuleta janga la watoto wa mitaani na ongezeko la makosa ya jinai pia mambukizi ya ukimwi kwa sababu ya baadhi ya wahanga kubainika kuambukizwa magonjwa hayo.
‘’mfano kwa mwaka 2019 jumla ya kesi 19 kwa kipindi cha mwezi janual hadi julay 2019 mchanganuo wake kama ifuatavyo kubaka kesi 3,mimba kwa wanagunzi kesi 3,shambulio la kudhuru mwili kesi 7,kujeruhi kesi 3,na kutelekeza familia kesi 2.’’alisema binyuara.
Aidha alilitaka jeshi la polisi kupitia dawati la kijinsia kushirikiana na taasisi hizo katika kukabiliana na majanga ya ukatili wa kijinsia kwa kutoa elimu sitahiki kwa jamii kwa lengo la kuifanya jamii yote kupata elimu na uelewa wa pamoja juu ya vitendo hivyo.
Mkurugenzi wa asasi inayojihusisha na utatuzi wa vikwazo vya maendeleo ya jamii-sucoda- ya mjini sumbawanga mkoani rukwa,samwel mwazyunga alisema mradi huo utaendeshwa katika kata nne za wilaya ya kalambo ili ili kukabiliana na changamoto za mila potofu.
‘’dhamira ya asasi yetu ni kuleta maendeleo endelevu katika jamii kwa njia ya ushirikishwaji wa wanajamii ili kuongeza uelewa katika maswala ya afya na mapambano ya dhidi ya ukatili wa kijinsia ,kukuza na haki za wanawake na watoto ,elimu ya lishe bora dhidi ya ukatili wa kinsia ,kukuza haki za wanawake na watoto ,elimu ya lishe bora utunzaji wa mazingira ,kilimo na ufugaji bora wa kisasa wa nyuki na mifugo mingine.’’alisema mwazyunga.
Mkurugezi mtendaji wa halmashauri hiyo msongera palela alisema mradi huo utasaidia kwa kutokomeza matukio ya ukatili wa kijinsia hususani katika maeneo ya vijiji na kuwataka viongozi wa miradi hiyo kushirikina na viongozi wa serikali za vijiji katika kuwapatia elimu kwa lengo la kuwafanya kuwa mabarozi kwenye maeneo yao husika.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.