Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Lazaro Komba amelitaka jeshi la polisi wilayani humo kuwasaka na kuwabaini wazazi na walezi wanaokatisha masomo ya watoto wao kisha kuwaozesha katika umri mdogo pamoja na kuwapeleka kufanya kazi za ndani kinyume na utaratibu.
Ameyasema hayo kupitia maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika ambayo kwa ngazi ya wilaya yamefanyika katika kijiji cha Kisumba wilayani humo na kuwataka wazazi na walezi kuwalinda watoto wao kwa kuwapatia huduma muhimu ikiwemo elimu,chakula na mavazi na kukemea tabia ya baadhi ya wazazi kuwakatisha masomo watoto kisha kuwapeleka kuchunga mifugo.
Mapema akiongea kupitia maadhimisho hayo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda amesema Halmashauri kupitia kitengo cha Ustawi wa jamii imejiwekea mikakati ya kuhakikisha watoto wanalindwa na kupatiwa stahiki muhimu katika jamii ikiwa ni pamoja na kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi yao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.