Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya kalambo Mkoani Rukwa Msongera Palela amezitaka Asasi zinazotekeleza miradi mbalimbali wilayani humo kukemea na kupinga mila potofu za wanawake kupakwa unga kichwani na kuwekewa sherehe kubwa pindi wanapokuwa wamepewa ujauzito kwa madai ya kuwa ni mashujaa.
Msongera ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi wa ukatili wa kijinsia unaotekelezwa na Asasi ya Sucoda,ambapo amesema baadhi ya mira wilayani humo zimekuwa zikiendekezwa na wananchi husani kwenye maeneo ya vijijini bila kujua athari zake.
Amesema kitendo cha wanawake kupakwa unga kichjwani pindi wapatapo ujauzito ni kitendo cha kibaya kwani kinahamasisha mimba za utotoni .
‘’anapopata ujauzito anashangiliwa kuwa yeye ni shujaa, sasa mira hizi ni potofu na ukizitazama mila kama hizi utakuta zinaendekeza mimba za utotoni ‘’alisema Msongera.
Amesema licha ya hilo mila hizo zimekuwa zikipelekea kujitokeza kwa vitendo vya utoro mashuleni kitu ambacho ni hatari kwa wanafunzi kuendelea na masomo hususani wa kike.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Daudi Sichone,amesema asasi zote hazinabudi kuungana na viongozi wa serikali za vijiji kwa kutoa mafuzo ambayo yatasaidia wao kuwaelimisha wananchi wao pindi wanakuwa kwenye mikutano ya hadhara.
‘’hatuwezi kurudi nyuma kimsisingi sisi kama halmashauri ya wilaya tuna jukumu la kuwasaidia wananchi kuondokana na chagamoto zinazowakabili.’’alisema sichone.
Vastina Valeli mwezeshaji wa mafunzo ya ukatili wa kijinsia amesema lengo ni kuhakikisha matukio ya ukatili wa kijinsia yanatokomezwa na kusaidia kuwajengea uwezo wakuu wa idara na watumishi wengine.
Mkuu wa wilaya ya kalambo Julieth Binyura amewataka wananchi kushirikina na dawati la ukatili wa kinsia katika kutoa taarifa sahihi juu ya uwepo wa matukio hayo ambayo yamekuwa yakikwamisha maendeleo katika jamii zao husika
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.