Halimashuri ya wilaya ya Kalambo imeungana halimashauri nyingine za mikoa y kanda ya kusini pamoja na taasisi mbalimbali katika maonesho ya kilimo ya nanenane yanayofanyika katika viwanja na John Mwakangale katika jiji la Mbeya. Maonesho hayo yalianza tarehe 01/08/2017 na yanatarajiwa kufikia kilele siku ya tarehe 08/08/2017. katika banda la Halimashauri ya wilaya ya Kalambo kuna bidhaa mbalimbali za wajasiliamali kutoka wilayani Kalambo ambazo zina mvuto wa kipekee kabisa, pia katika banda letu kuna wataalamu wa kilimo na ufugaji ambao wanatoa elimu ya mbinu bora za kilimo cha mazao mbalimbali na mbinu bora za ufugaji
Mmoja wa wataalamu wa kilimo kutoka Kalambo akielezea zao jipya ya Beet roots ambalo linaaminika kuongeza damu mwilini
Katika banda la Halimahsuri ya wilaya ya Kalambo kuna mjasiliamari ambaye anatengeneza viatu vya ngozi kutoka Kalambo,viatu vyake vinavutia sana na ni vya kudumu, viatu hivyo anaviuza kwa bei rahisi sana ukilinganisha na ubora wa bidhaa hiyo.
Hizi ni baadhi ya Bidhaa za wajasiliamali zinazopatikana katika banda la Halimashauri ya wilaya ya Kalambo
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.