Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, imefanikiwa kukusanya fedha za mapato ya ndani kiasi cha shilingi billion 2.2 hadi kufikia tarehe 26 June 2025.
Mafanikio hayo yamechangiwa na udhibiti wa mianya ya utoroshaji wa mazao kwa kuweka CCTV camera katika mageti 7 ikiwa ni Pamoja na kuunda kamati maalumu za ufuatiliji na udhibiti upotevu wa mapato.
Mkuruegenzi mtendaji wa mtendaji wa Halmashauri hiyo bwana Shafi Mpenda amesema Pamoja na mafanikio hayo, Halmashauri hiyo katika mwaka wa fedha 2025/2026 imejipanga kuongeza vyanzo vipya vya mapato ambavyo vitasaidia Halmashauri kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa wakati.
Sambamba na makusanyo hayo, Bwana Shafi Mpenda amebainisha kuwa serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi million mia tatu (300,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi wa soko jipya la wafanyabiashara wadogo lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 200.
Hata hivyo katika mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ilikadiria kukusanya Mapato ya Ndani kiasi cha Shilingi 2,412,405,000.00 ambapo hadi kufikia Mwezi Juni 2024 kiasi cha Shilingi 1,935,099,446.00 kilikusanywa sawa asilimia 80% ya makisio.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.