Jamii mkoani Rukwa imeashauliwa kujenga mazoea ya kupima afya zao kupitia vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya sambamba na kujiunga na bima afyailioboreshwa CHF ambayo inajumaisha watu sita wa familia moja na kugharimu kiasi cha shilingi elfu therathini.
Mfuko wa bima ya afya ilioboreshwa ulianza kwa mara ya kwanza kutumika Mkoani Dodoma mwaka 2012 na baadae kupelekwa kwenye mikoa ya morogoro na shinyanga mwaka 2015 na huku ukitekelezwa chini ya sheria namba1ya CHFya mwaka 2001na kuhudumu ndani ya halmashauri167kati ya halmashauri 185 hapa nchini.
Licha ya hilo lengo kubwa la uanziswaji wa mfuko huo ilikuwa ni kutoa huduma bora kwa wananchi zenye gharama nafuu na kuhakikisha upatikanaji wa huduma kuanzia ngazi ya zahanati mpaka ngazi ya hospitali ya rufaa ya mkoa kwa kuzingatia utaratibu zinapatika kwa urahis zaidi kama
Awali akiongea kupitia mafunzo ya CHF yalijumisha watendaji wa vijiji , waratibu elimu kata pamoja na wahudumu wa vituo vya kutolea huduma za afya mganga mkuu wilayani humo Alen Mlekwa amesema lengo ni kuwapatia elimu juu ya mfuko huo.
Amesema lengo la serikali ni kuwasaidia wananchi kuondokana na adha ya kupata matibabu kwa gharama kubwa na kusema endapo kila mwanachi atachukua hatua zaidi juu ya swala hilo kwa kujiunga na bima ilioboreshwa atakuwa na uwezo wa kutibiwa mahali popotendani ya mkoa husika.
Amesema bima ilioboreshwa inafaida nyingi kutokana na kwamba mtu anaweza kutibiwa mahali popote bila budha na kuitaka jamii kuchangamikia fulsa hiyo .
Akiongea na wananchi wa kata ya samazi wilayani humo mganga mkuu wa mkoa huo Bonifas Kasululu, amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata tiba bora na kwa bei nafuu na kuwasihi wananchi kuendelea kujiunga na bima ilioboreshwa kwa lengo la kuzisaidia familia zao pindi zinapopata matatizo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa walengwa zaidi wa mfuko huo itawa ni familia zenye kipato cha chini na zilizo kwenye mfumo usiokuwa rasmi
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.