Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa imepata hati safi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 baada ya kufanya vizuri katika maeneo tofauti ikiwemo matumizi na ukusanyaj wa fedha,usimamizi wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imeonesha kuwa taarifa za fedha, usimamizi wa miradi na usimamizi wa mapato zilizingatia sera za kihasibu na kufuata matakwa ya viwango vya kihasibu vya kimataifa kwa sekta ya umma.
Hata hivyo imeelezwa kuwa katika taarifa zilizokuwa zimewasilishwa kwenye Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 zilikuwa sahihi na za kueleweka ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa ulinganisho wa Mwaka wa Fedha uliopita (2018/2019) na kwamba taarifa zote zilionesha utoshelevu wa maswala yote muhimu yanayo husu Taarifa za Fedha.
Kwa mujibu wa Mkaguzi wa Hesabu za Ndani katika Halmashauri ya Kalambo (CPA. Haji Mussa Chewa) amebainisha kuwa Halmashauri ya Kalambo imepata hati Safi kutokana na kuzingatia Viwango vya Kimataifa vya Uandaaji wa Hesabu za Umma na kufuata ushauri wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Halmashauri ya Kalambo ilianzishwa 23 Disemba mwaka 2012 kwa kumegwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga na kutangazwa kuwa Halmashauri January 2013 kwa tangazo la serikali (GN 631)
Hata hivyo Halmashauri hiyo ilianza kutekekeleza bajeti rasmi kuanzia tarehe 1 Julai, 2013 licha ya kuwa ilianza kazi zake tarehe 23 Machi 2013 baada ya kuundwa kwa baraza la kwanza la madiwani.
Aidh Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ilipata Hati isiyoridhisha katika Mwaka wa Fedha 2014/2015 na katika Mwaka wa Fedha 2013/2014 ilipata Hati Safi na ndio mwaka ambao Halmashauri ilianzishwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.