Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imesema imetenga million arobaini(40,000,000) kwa ajili ya umaliziaji wa kituo cha fya kanyezi ikiwa ni jitihada za kuwezesha wananchi katika maeneo hayo kuondokana na adha ya kutafuta huduma za matibabu mbali na maeneo yao.
Mapema akiongea na kituo hiki mwenyekiti wa halmashauri hiyo Daud Sichone amesema katika kuwezesha wananchi kuondokana na adha ya kutafuta matibabu mbali na maeneo hayo halmashauri imetengewa million 40,000,000 kwa ajili ya kukamilisha majengo ya kituo hicho.
‘’katika mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri imetengewa jumla ya Tsh. 40,000,000 ili kukamilisha majengo yote na kuanza kutoa huduma kwa kuwa pia kituo hiki kimesajiliwa katika mifumo ya upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na huduma za basket fund.’’ Alisema sichone.
Mapema akiongea wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo kaimu mkuu wa idara ya ujenzi katika Halmashauri hiyo mhandisi Jackson Mtegu alisema mwaka 2018 halmashauri ilipokea million mia nne 400,000,000, kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kanyezi na kujumuisha majengo manne ikiwemo jengo la wagonjwa (OPD) jengo la upasuaji ,jengo la maabara na jengo la RCH.
‘’ ujenzi umefikia asilimia 80% kazi ambazo hazijakamilika ni mfumo wa maji safi na maji taka na mfumo wa umeme ’’alisema Mtegu
Hata hivyo hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga alifanya ziara ya ukaguzi wa kituo hicho na kutoa siku 14 kuanza kwa umaliziaji wa kituo hicho.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.