KATIBUmkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi),Joseph Nyamuhanga ametoa siku 90 kwa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa kuhakikisha inaanza ujenzi wa kituo cha afya Samazi vinginevyo itanyang'anywa fedha zilizotolewa kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho.
Agizo hilo alilitoa hivi karibuni alipokuwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujezi wa vituo vya afya pamoja na hospitari za wilaya katika mkoa wa Rukwa.
Alisema kuwa serikali ilitoa fedha muda mrefu, kiasi cha shilingi milioni 400 kwaajili ya ujezi wa kituo hicho cha afya lakini mpaka sasa ujezi wake haujaanza kitendo ambacho ni kuchelewesha huduma kwa wananchi.
"Serikali imetoa maelekezo na sio muanzi tena marumbano ya wapi kijengwe kituo hicho kama mtaendelea na hali hii mtanyang'anywa fedha hizo wapewe wengine wanao zihitaji na wako tayari kutekeleza maelekezo ya serikali kwa wakati" alisema
Aidha alielekeza kuwa kwakuwa katika Kijiji hicho tayari kuna zahanati , nibora iliopo ipanuliwe ili kuwe na majengo mengi ambayo yatakidhi mahitaji ya sasa ambapo ilichopo imeonekana ni ndogo kutokana na idadi ya watu waliopo wakati huu.
Aidha alisema kuwa serikali inategemea kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni 300 kwa kila hospitali ya wilaya kwa ajili ya kukamilisha ujenzi na aliwaagiza wakurugezi nchi nzima kuzitumia fedha hizo vizuri ili zikidhi mahitaji.
Hata hivyo imeelezwa kuwa zaidi ya vituo vya afya 350 vipya vimejengwa nchi nzima na vituo vingine 67 vinatarajiwa kujengwa ifika mwaka 2020.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.