Waamini pamoja na wachungaji kutoka madhehebu mbalimbali ya dini kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wameungana kuendesha kongamano la kumuomba mwenyezi Mungu ili uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu,uwe wa haki ili kuilinda amani na utulivu uliopo kwa lengo la kuivusha nchi ikiwa salama bila kumwaga damu.
Makamu askofu wa kanisa la FPCT jimbo la Rukwa na katavi Andrea Mwakalinga amesema watumishi wa Mungu tunahitaji kamapeni safi bila ugomvi na kwamba kufanya fujo ni kukosa hekima ya kimungu.
Amesema kwa kuwa wagombea wote wanatoka katika makanisa na misikiti yetu, Mashehe na Wachungaji tuta hakikisha tuna hubiri amani na utulivu kwenye mihadhara yetu.
‘’sisi tuna watu wengi wanao tufuata makanisani na misikitini mwetu, hivyo hatunabudi kuhimiza upendo ili zifanyike kamapeni zisizo na ugonvi kwenye majukwaa ya siasa. Na ijulikane kuwa mtu yeyote atakaye fanya kampeni za fujo kuelekea uchaguzi huu, atakuwa hana nia njema katika ustawi wa nchi yetu.’’ Amesema mwakalinga.
Shehe wa wilaya hiyo Sulemani Amani, alisema kila mtu amefika katika eneo hilo kwa lengo la kufanya maombi na kuwataka washirika wote kuomba katika roho na kweli ili kuhakikisha maombi hayo yanafika kwa mwenyezi mungu kama ilivyo kusudiwa.Mkuu wa wilaya ya Kalambo Calorius Misungwi, amesema kila mwananchi anatakiwa kuchagua viongozi bora baada ya kusikiliza sera zao.
‘’Sisi kazi yetu kama wananchi ni kusikiliza sera na kuchagua viongozi wenye sifa safi. Hivyo wote tuhamasike na tujitokeze kwa wingi kuchagua viongozi bora ambao watakuwa msaada kwa wilaya na taifa kwa ujumla.’’ Amesisitiza Misungwi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.