...Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo wamepata mafunzo juu ya utumiaji mfumo mpya (ulioboreshwa) wa kupanga, kubajeti, na kuripoti (PlanRep Web Based) katika ukumbi wa Sunrise, Matai. Mafunzo hayo ya siku tatu yalianza tarehe 26 hadi 28 Septemba 2017 yakiendeshwa na baadhi ya Maafisa wa Halmashauri hiyo waliohudhulia mafunzo ya awali ya mfumo huu katika kanda ya Kigoma. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo Maafisa wa Halmashauri hiyo juu ya mfumo huo ambao utakua unapatikana kupitia kiambaza (browser) katika kompyuta.
Awali mafunzo hayo yalifanyika katika kanda mbalimbali Nchini ambapo Maafisa Mipango, Waweka Hazina, Waganga Wakuu, Maafisa TEHAMA pamoja na Makatibu wa Afya walipatiwa mafunzo juu ya mfumo huo na kupewa jukumu la kufikisha elimu hiyo kwa Maafisa mbalimbali waliobaki katika Halmashauri zao
Mfumo mpya wa PlanRep (PlanRep Web Based) ni mfumo ambao umefanyiwa maboresho makubwa kwa kuchukua mazuri yaliyopo katika PlanRep ya awali na kuongeza mengine kwa lengo la kuboresha na kurahisisha zoezi la upangaji bajeti katika Halmashauri zetu. PlanRep mpya itasaidia upatikanaji wa taarifa moja ya bajeti husika (kuondoa ufanyaji mabadiliko katika bajeti mara baada ya kutuma kwenda ngazi nyingine) kwa kila ngazi kutokana na kuwepo udhibiti wa kutosha.
Kupitia Matumizi ya Planrep iliyoboreshwa itarahisisha uandaaji na upatikanaji wa bajeti katika Halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na kuziondolea gharama kubwa iliyokua ikitumika katika zoezi la kuandaa bajeti, gharama ambazo zilizotokana na matumizi makubwa ya uchapishaji karatasi, gharama ya safari,na posho za kuwasilisha bajeti katika ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, fedha ambazo kwa sasa zitatumika katiaka utekelezaji wa shughuli nyingine za Halmashauri.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.