Rais wa Tanzania, John Magufuli ametoa tahadhari kuhusu ugonjwa unaotokana na virusi vya corona, akiwataka kutopuuza kwani mpaka sasa umegharimu maisha ya watu wengi duniani.
Amezungumza na Umma wa Tanzania alipokuwa akizindua karakana kuu ya Jeshi la Wananchi Tanzania hii leo jijini Dar Es Salaam.
Katika kusisitiza tahadhari iliyotolewa hivi karibuni na Waziri wa afya nchini humo, Ummy Mwalimu, Rais Magufuli amewataka raia kutopuuza tahadhari hizo.
''Ugonjwa upo na umekumba nchi nyingi kwa takwimu zilizopo ni kwamba zaidi ya watu 100,000 wameambukizwa na watu 4,500 wamepoteza maisha.''
''Tunatambua kuwa Tanzania mpaka sasa hatuna mgonjwa wa corona lakini hatuwezi kujiweka pembeni bila kuchukua hatua, na hatua zimeanza kuchukuliwa Waziri wa wizara ya afya ameshatoa tahadhari tunazopaswa kuchukua''.
''Ugonjwa huu unaua na unaua kwa haraka, sana niwaombe tusipuuze, tusipuuze hata kidogo ni lazima kuchukua hatua za kujikinga na tatizo hili.''
kwa wale wanaopenda kusafiri safiri sana kama safari si ya lazima usisafiri, lazima kuwe na sababu ya lazima ya kusafiri. umefika wakati wa kudhibiti safari zetu kwa ajili ya kujilinda na tatizo hili.
''Zile tahadhari tunazopewa tusizipuuze, ni vyema kuchukua tahadhari, kila mmoja kwenye familia yetu tutoe tahadhari na elimu, mashuleni, vyuoni, makambini, jeshini kwenye magari, tuweze kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini mwetu''.
Vyombo vya habari, nyumba za starehe, nyumba za ibada vimetakiwa kuwa na utaratibu wa kuwa na angalau maneno mawili ya kusema kutoa elimu kuhusu virusi vya corona kila wakati.
Kuahirishwa kwa safari za ndege kwenda India
Rais Magufuli amesema kuwa katika hatua ya kudhibiti kuingia kwa maambukizi ya virusi nchini Tanzania, nchi hiyo pia inapunguza taratibu za safari.
amesema ndege iliyokwenda India jana ikirejea nchini Tanzania haitafanya safari tena, kutokana na hali ya nchi mbalimbali kujiweka katika karantini.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.