Bodi ya michezo ya kubahatisha nchini kwa kushirikiana na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani Rukwa na Katavi imekamata na kuteketeza kwa moto mashine 24 za michezo ya kubahatisha zenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 46 na kupiga malfuku watoto kuhusishwa kwenye michezo hiyo.
Mashine hizo ambazo nyingine ziligundulika kuwa feki na baadhi zikiwa zimeingizwa nchini kinyemela bila kufuata utaratibu ,zilikamatwa kwa nyakati tofauti na kuteketezwa kwa moto katika mikoa ya Katavi na Rukwa.
Katika mkoa wa Katavi ,mashine nane zenye thamani ya shiingi milioni 12 zilikamatwa wilayani Mlele katika mji wa Inyonga katika kiijji cha Majimoto na kuteketezwa kwa moto.
Katika mkoa wa Rukwa zilikamatwa mashine 16 zenye thamani ya shilingi millioni 30 katika vijiji vya mwambao wa Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga .Mkurugenzi mkuu wa bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania , Jemes Mbalwe, jana alisema serikali imeweka utaratibu wa kisheria wa uingizaji wa vifaa mbalimbali kutoka nje ili iweze kunufaika kupitia ukusanyaji kodi.
‘’sekta hii imekuwa ikichangia sehemu kubwa ya mapato ya nchi yetu,kwa mwaka wa fedha 2019 /20 pekee imechangia Zaidi ya shilingi billion 95 katika pato la taifa ‘’alisema.
Alieleza kuwa kwa mujibu sheria,mashine hizo zinatakiwa kuwekwa katika maeneo ya kuuzia vileo,nyumba au maduka maalumu yaliosajiliwa na waendeshaji kulipa kodi.
Meneja wa TRA mkoani Rukwa Chacha Boazi , alisema msako huo ni endelevu ili kuwabaini wanao kwepa kulipa kodi kwa kutumia mashine feki na zinazoingizwa nchini kinyemela bila kusajiliwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.