Mawakala wa vyama vya siasa Nchini wametakiwa kutoingilia mchakato wa uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura vituoni na badala yake wazingatie Sheria za uchaguzi na kanuni za uboreshaji maelekezo ya tume na kusimamia miiko na mipaka ya uendeshaji zoezi la uboreshaji daftari.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa tume huru ya uchaguzi Nchini wakati wa mkutano na wadau Mkoani Rukwa na kuwakilishwa na Ndugu Martin Mnyenyelwa na kusisitiza mawakala kutumia taratibu zilizo ainishwa katika Sheria zinazo simamia uchaguzi na kuziwasilisha changamoto zao kwenye tume kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.
Amesema uboreshaji wa daftari unalenga kuwaandikisha raia wa Tanzania waliotimiza umri wa miaka 18 na zaidi au watakao timiza umri huo wakati wa tarehe ya uchaguzi wa mwaka 2025 na ambao hawajapoteza sifa kwa mujibu wa Sheria ya uchaguzi.
Aidha alisisitiza Wananchi Mkoani humo kujitokeza kwa wingi wakati wa uboreshaji taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Hata hivyo maandalizi ya uboreshaji daftari la wapiga kura katika mzunguko wa 9 kati ya mizunguko 13 yanafanyika katika Mikoa ya Rukwa ,Songwe na Ruvuma huku kauli mbiu ya uboreshaji daftari la wapiga kura kwa mwaka 2025 ikiwa ni’’,kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora’’.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.