Mbunge Jimbo la Kalambo Josephat andege amesema bei ya mahindi imeongezeka kutoka shilingi 600 ya bei ya awali hadi kufikia shilingi 900 sawa na ongezeko la shilingi 300 kwa maeneo ya mjini na shilingi 200 kwa maeneo ya vijijini.
Aliyasema hayo kupitia mikutano ya hadhara aliyoifanya katika maeneo ya vijiji vya Singiwe, Katuka,Msanzi,Mau na Kanyalakata na kuwataka wananchi wilayani humo kuacha tabia ya kuuza mazao yao kwa bei ya hasara na kusema lengo la serikali ni kuwawezesha wakulima kunufaika na kilimo.
Aidha aliwakikishia wananchi wilayani humo kupata mbolea ya ruzuku kabla ya msimu kuanza kutokana na serikali kuweka mazira rafiki ambayo yatawezesha mbolea kuwafikia wakulima katika maeno yao husika.
Licha ya hilo Kandege alifanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendelo katika kijiji cha Katuka na kuwakikishia wakazi wa vijiji vya Singiwe na chalaminwe kumalizia ujenzi wa zahanati ,shule ya msingi pamoja na jengo la ofisi ya chama cha mapinduzi ambalo linajengwa kwa nguvu za wanachama.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.