HALMASHAURI ya Kalambo mkoani Rukwa imesema imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 140 katika bajeti ya 2020/ 2021 kwaajili ya umaliziaji wa maboma ya majengo yote ya zahanati
Akiongea ofini kwake kaimu Mkurugenzi wa Halmashuari hiyo Magreth Kakoyo, alisema katika maboma yaliyobakia Halmashauri inaendelea kufanya maandiko ili kuhakikisha yanakamilika na kutoa matunda kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.
‘’Halmashauri katika bajeti ya mwaka 2020/2021imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 140 kwa ajili ya umaliziaji wa maboma yote ya zahanati ikiwemo na maboma ya vijiji vya Tunyi, Mzungwa na Ilonga kwani vijiji hivi viko mbali na makao makuu ya Wilaya na kata husika haina kituo cha afya,
‘’Niendelee kuwahimiza wananchi waendelee kujitolea nguvu kazi kwenye kufyatua na kuchoma tofali, kusogeza mawe na mchanga pamoja na kujenga walau kufikia usawa wa linta kwani kipaumbele cha sasa ni kukamilisha maboma yaliyojengwa na wananchi wenyewe.’’ Alisisita na kuwaomba wananchi katika maeneo hayo kuendelea kuwa wavumilivu.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi katika kata ya Mambwenkoswe juu ya maeneo hayo kuwa na upungufu wa vituo vya kutolea huduma za afya na huku kata hiyo ikiwa na zahanati moja licha ya kuwa na vijiji sita .
Diwani wa kata hiyo Juliasi Kanowalya ,alisema wananchi wake wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika zahanati ya Kalembe ambayo inategemewa na kata nzima .
Alisema baadhi yao wamekuwa wakilazimika kitibiwa katika nchi jirani ya Zambia kutokana na vijiji vyao kuwa na umbali wa zaidi ya km kumi kutoka kwenye maeneo ya kutolea huduma za afya.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.