Halmashauri ya Kalambo mkoani Rukwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imefanikiwa kutenga fedha million 196,000,000/= kwa ajili ya ukamilishaji majengo katika Hospitali ya wilaya ikiwemo vituo vya afya na Zahanati ambapo kati ya fedha hizo million 70,000,000 /= zimetengwa kukamilisha wodi tatu katika Hospitali ya wilaya na 126,000,000/= kukamilisha vituo vya afya Pesa hizi kutoka mapato ya ndani.
Mkurugezni mtendaji wa Halmshauri hiyo Shafi Mpenda alisema Lengo kubwa ni kuhakikisha Hospitali hiyo inafanya kazi kwa asilimia miamoja na kwamba mpaka sasa majengo yaliokamilika ni pamoja na jengo la wagonjwa wa nje (OPD),nyumba tatu za watumishi, Jengo la (mionzi x-ray), Jengo la kuhifadhia maiti (mortuary) jengo la kufulia (laundry) na jengo la wazazi (maternity).
Aidha alisema majengo yanayorajiwa kukamilishwa kupitia fedha hizo ni pamoja na jengo la Wodi ya watoto ,Wodi ya wanawake na Wodi ya wanaume na kwamba lengo la serikali ni kuhakikisha majengo yote ifikapo mwishoni mwa mwezi wa nane yawe yamekamilika na kuanza kutoa huduma na kwamba mpaka sasa huduma zimeanza kutolewa kwa wagonjwa wa nje.
Hata hivyo akiongea kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la Santamalia wilayani humo Mbunge wa jimbo hilo Josephati Kandege, aliagiza kukamilishwa haraka kwa majengo hayo ili kuruhusu wananchi kupata matibabu kwa karibu na maeneo yao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.