Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amewaagiza wakuu wa Wilaya Mkoani humo kusimamia tathmini ya utekelezaji wa mkakati wa miaka mitano (2020 -2025) wa kukabiliana na mimba za utotoni na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa watoto wenye umri chini ya miaka 8.
Mh. Wangabo ameagiza kuwa tathmini hiyo ifanyike mwezi Januari 2021 katika ngazi ya Wilaya na Mwezi Februari, 2021 katika ngazi ya Mkoa ili kubaini mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja tangu mkakati huo kuzinduliwa tarehe 18.2.2020
Aidha, alitaja baadhi ya mambo muhimu aliyowasainisha wakuu hao wa wilaya kuwa ni Pamoja na ujenzi wa shule za msingi kwa kila Kijiji, chakula mashuleni, ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za sekondari na kila kata kuwa na shule yake ya sekondari.
Mh. Wangabo ametoa maagizo hayo wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Kuzuia Ndoa na Mimba za Utotoni Mkoani Rukwa huku ukiwa na lengo la kuwawezesha Watoto wa kike kutambua haki zao, kujikinga dhidi ya ndoa za utotoni, kuimarisha mifumo ya ulinzi na haki kwa Watoto Pamoja na kukabiliana na mila potofu.
Hivi karibuni mashirika yasiokuwa ya kiserikali ikiwemo ECD kwa kushirikiana na wadau wengine wamekuwa msitari wa mbele kupinga matukio ya ukatili dhidi ya watoto wenye umri chini miaka 8 .
Uzinduzi mradi huo ni mwendelezo wa kutekeleza mkakati wa miaka mitano (2020 – 2025) wa kukabiliana na mimba za utotoni Mkoani humo kama alivyoahidi katika salamu zake za kufunga mwaka 2019 kuwa mwaka 2020 utakuwa ni mwaka wa mtoto mkoani Rukwa huku mradi huo ukilenga kuwafikia Watoto 32,167; wasichana wakiwa 22,356 na wavulana 9,811. Pia walezi na wazazi 21,881 katika wilaya 3, Kata 36 na vijiji 116.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.