Mkuu Wa Wilaya Ya Kalambo Akelwa Ukosefu Wa Huduma Ya Maji Katika Mji Wa Matai.
Posted on: June 24th, 2019
Wananchi katika kjiji cha kisungamile kata ya matai wilayani kalambo mkoani Rukwa wameiomba serikali kufanya marekebisho ya miundombinu ya maji ambayo imeharibiwa na mifugo na hivyo kupelekea kukosekana kwa huduma hiyo muhimu kwa zaidi mwezi mmoja na hivyo kulazimika kutumia maji ya visima ambayo ni hatari kwa afya zao.
Kijiji cha kisungamile kina zaidi ya wananchi elfumoja 1000 na kina patikana katika kata ya matai wilayani hapa,licha ya hilo kijiji hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma ya maji na huku wananchi wake wakilazimika kutumia maji ya mto chimilango pamoja na maji ya visima ambayo si salama kwa afya zao na hivyo kulazimika kuitisha mkutano wa hadhara ili kujua hatima ya swala hilo.
Mmoja wa waananchi wa kijiji hicho jeradi swetu akiongea mbele ya mkutano wa hadhara, alisema serikali kupitia halmashauri hiyo haina kufaanya marekebisho ya miundombinu ya maji kuzunguka maeneo hayo.
‘’wakati mwingine maji utakuta yanatoka na wakati mwingine utakuta maji hayatoki hususani kwenye maeneo ya mji wa matai , sasa ningeomba serikali ifanye jitihada za kuhakikisha maji yanbatoka muda wote’’alisema Swetu.
Nikas mchefya mkazi wa kijiji hicho, alisema katika maeneo hayo kuna miradi miwili ya maji lakini miradi yote haitoi maji na kusema tatizo kubwa ni kutokana na mabomba ya maji kukatwa na wafugaji kutokana na mabomba hayo kupitishwa juu sana.
‘’Wafugaji wanapokuwa wakipishwa mifugo yao mara nyingi hujikuta wakikata mabomba kwa bahati mbaya ‘’alisema mchefya.
Diwani wa kata hiyo Vitus Tenganamba alisema serikali inampango wa kuanzisha mradi mpya wa maji kwenye maeneo hayo na kuwataka wananchi kuendelea kuwa na subira wakati swala lao likiendelea kufanyiwa kazi.
Mkuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura alilazimika kuingilia kati swala hilo na kuwataka wananchi kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la kuondokana na adha kuziba kwa mabomba hususani wakati wa masika
‘’Wananchi wangu hata watu wanaolima kule milimani nao wanachangia kwa kiasi kikubwa maji kutoka na matope kwani hata yakitoka watu wanashindwa hata kufulia nguo sasa ni vizuri mkaacha tabia ya kulima huko milimani hususani kwenye vyanzo vya maji.’’alisema Binyura.
Hata hivyo imeelezwa kuwa chanzo cha kukatika kwa maji kila wakati kwenye maeneo hayo ni kutokana na wananchi kulima kwenye vyanzo vyamaji na huku maji yanayotoka yakiwa ni machafu muda wote.