Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Julieth Binyura amewaamuru wananchi wote katika kijiji cha Kipwa kilichopo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Zambia kuhamia katika maeneo ya miinuko kufuatia kijiji hicho kuzingirwa na maji ya ziwa Tanganyika na kusababisha baadhi yao kukosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka.
Hatua hiyo imekuja baada ya wakazi ya kijiji hicho kuiomba serikali kuweka huduma ya maji pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara katika maeneo mapya ya milima ya mawe Sande ambako wanatarajia kuhamia hivipunde kufuatia kijiji chao kuzingirwa na maji ya ziwa Tanganyika na kupelekea baadhi yao kukosa makazi kutokana na nyumba kubomoka.
Wamesema tatizo kama hilo liliwahi kutokea mwaka 1984 na kujitokeza tena mwaka huu ambapo nyumba kadhaa zimebomoka na kusababisha hasara kubwa.
‘’tunaiomba serikali kuangalia namna ya kutusaidia kupata huduma ya maji pamoja na kupasua barabara inayotokea Katika maeneo ya Mpombwe, ili kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa kwa njia ya magari tofauti na hivi sasa ambapo wanalazimika kutumia boti kupitia ziwa Tanganyika.
Kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama, Kaimu Meneja wa RUWASA Wilayani Kalambo Fransis Mapunda, alisema Serikali inapeleka miundo mbinu ya maji safi na salama kijijini Kipwa na maeneo mengine ya mwambao wa ziwa Tanganyika kufuatia uwepo wa vyanzo vya maji ambavyo ni vya uhakika.
Akiongea ofisini kwake, mkuu wa wilaya ya Kalambo Jilieth Binyura, alisema serikali ina mpango wa kupeleka huduma ya maji pamoja na kuboresha miuondombinu ya barabara na kuwasihi wananchi kuwa na subira.
Aidha aliwasihi kuendelea kuhamia katika maeneo ya miinuko ili kuepukana na adha ya nyumba zao kubomoka kutokana na maji kuzingira maeneo yao.
Alisema kubomoka kwa nyumba katika kijiji cha Kipwa kumesababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo imepelekea maji ya ziwa Tanganyika kujaa na kuvamia nyumba za watu hatimaye baadhi yao kukosa makazi.
‘’niwasihi wananchi wote kuacha tabia ya kukata miti ovyo na kuharibu uoto wa asili na hivi sasa ambao wanaona wako maeneo ya mabondeni ambayo ni hatarishi waanze kuhamia maeneo ya miinuko.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.