...Zoezi la uboreshaji Mtandao Kiambo (Local Area Network) katika Majengo ya Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) lakamilika. Zoezi hilo lilichokua muda wa wa siku saba limekamilika Tarehe 29/01/2017 ambapo Meneja Wa Mradi Mkoa wa Rukwa Bi. Rose Mangilima amekabidhi uboreshaji huo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Injinia Simon Ngagani. Aidha Mkurugenzi Mtendaji Injiania Simon Ngagani amemshukuru meneja wa mradi wa PS3 pamoja wataalam waliofanya kazi hiyo na kuwakaribisha Wilaya ya Kalambo pale walipokua wakimuaga mara baada ya kukamilisha zoezi hilo Tarehe 31/07/2017.
Uboreshaji huu wa Mtandao kiambo utasaidia upatikanaji wa mifumo mbalimbali ya TEHAMA katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo ambapo maeneo ya Idara ya Fedha, Mipango na Ufuatiliaji, Utawala, pamoja na TEHAMA yalipewa kipaumbele.
Katika kuboresha mifumo ya TEHAMA katika sekta ya Umma, Mradi wa PS3 unaendelea na maboresho katika mfumo wa kielektroniki wa Ukusanyaji Mapato (LGRCIS), Mfumo wa Kupanga na kuripoti bajeti (PlanRep), tovuti za Serikali pamoja na baruapepe za watumishi wa Umma pamoja na Mtandao Kiambo (LAN)
Mbali na Uboreshaji mifumo ya TEHAMA Mradi wa PS3 ambao unafadhiriwa na Watu wa Marekani (USAID) unafanya maboresha katika sekta ya Utawala Bora, Rasilimali Watu, Rasilimali Fedha pamoja na Tafiti Tambuka.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.