Kumekwepo na changamoto ya baadhi ya watendaji kuto lejesha fedha za vitambulisho vya ujasilimali licha kutoa vitambulisho hivyo kwa wafanyabishara na kupatiwa fedha na hivyo kupelekea uongozi wa wilaya hiyo kuanzisha oparesheni ya ukaguzi wa vitambulisho hivyo kupitia kwa watendaji na kubaini baadhi ya watendaji kula fedha hizo kinyume na utaratibu.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo katibu tawala wilayani humo Frank Schalwe,amesema wamelazimika kuchukua hatua ya kumweka ndani mtendaji wa kijiji cha Mau baada ya kula fedha za vitambulisho kiasi cha shilingi million moja na elfu themani.
‘’mkurugezi amekuwa akitoa taarifa mara kwa mara juu ya kutolewa kwa vitambulisho fedha zimekuwa hazionekani licha ya vitambulisho kutolewa kwa wingi na ndio maana tukaanzisha masako wa kata kwa kata na kubaini baadhi ya watendaji kuzitafuna fedha zavitambulisho’’alisema sichalwe .
Alisema mtendaji huyo ataendelea kushikiliwa na jeshi la polis mpka pale atakapo lipa mkuu wa wilaya atakapo kuwa amerudi kutoka safari.
Mkurugezi mtendaji wa halmashauri Hiyo Msongela Palela amewaonya watendaji kuacha tabia ya kuzitumia fedha za vitambulisho katika matumizi yao binafus na kusema atakae bainika hatua kali za kishera dhidi yake zitachukuliwa.
‘’hizi fedha za vitambulisho msizile watendaji wangu ni bora mle fedha zingine lakini si hizi,nawaonya acheni mchezo huo kwani ni baya ‘’alisema palela.
Aliidha alitumia fulsa hiyo kuwasihi watendaji kuendelea kuwa wanifu hususani wakati wa ukusanyaji fedha za vitambulisho hivyo na kusema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuondokana na matatizo yasio kuwa ya lazima.
Hata hivyo serikali ilitoa vitambulisho elfu kumi na tatu namia mbili hamsini na huku mpaka sasa vitambulisho 3065 vikiwa vimetolewa kwa wafanya biashara.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.