Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoani Rukwa Silafu Maufi ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kalambo kuweka mkakati wa kudhibiti vitendo vya utoro kwa wanafunzi wa shule za msingi ikiwemo kufanya vikao na walimu pamoja na wazazi na walezi.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara katika shina namba 10 katika kijiji cha Mikonko wilayani Kalambo kisha kupokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi na kuwataka wakazi maeneo hayo kuendelea kuunga mkono serikali kwa kuchukua jukumu la kuwapeleka watoto shule ikiwemo kuisaidia serikali katika kudhibiti utoro wa wanafunzi shuleni.
Licha ya hilo aliwataka wananchi kujenga mazoea ya kupanda miti ya matunda na miti ya mbao ambayo itawezesha kujikwamua na hali ya kiuchumi
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.