Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah ulega ameyaagiza mashamba yote kumi na minne ya mifugo nchini-Ranchi- kuanza kutumika kwa ajili ya kutoa mafunzo endelevu ya malisho bora ya mifugo ya wafugaji.
Ulega amemweleza mwenyekiti wa bodi ya mashamba ya mifugo nchini –Narco-, Paul kimiti aliyeshiriki kikao cha wafugaji wa mifugo ya shamba la kalambo lililoko wilaya ya kalambo mkoani Rukwa kuwa mafunzo hayo yatakuwa na tija kwa ustawi wa mifugo na kutoa mwongozo wa kuanzishwa mafunzo ya ufugaji bora katika mashamba ya mifugo nchini-ranchi-kwa wafugaji wanaopewa vitalu vya kulishia mifugo yao kwenye mashamba hayo.
Amesema utaratibu unaotumika hivi sasa wa kuwamilikisha wafugaji vitalu vya kulishia mifugo yao bila ya kuwaelekeza njia bora na sahihi ya ulishaji bora wa mifugo unashindwa kuwavutia wagufaji hao kuibaini tofauti iliyopo ya kuzitumia huduma na fursa za mashamba hayo.
mwenyekiti wa bodi ya mashamba ya mifugo nchini-narco-, paul kimiti amesema wakati umefika kwa mashamba ya mifugo nchini kuonyesha tofauti ya ufugaji wa kisasa wenye tija.
Mkuu wilaya ya kalambo Julieth Binyura amemweleza naibu waziri uhusiano uliopo kati ya wavuvi wanaolitumia hususani katika ziwa Tanganyika na wavuvi wa nchi jirani ya Zambia.
Naibu waziri wa mifugo na uvuvi aliyekuwa na ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Rukwa ameweza kukutana na wafugaji na wavuvi katika halmashauri zote nne za mkoa huo na kujadiliana njia bora na sahihi za kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia sheria za nchi.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.