Naibu waziri wa ujenzi Mh. Godfrey Kasekenya amefanya ziara ya ukaguzi wa barabara ya Matai -Kasesya wilayani Kalambo mkoani Rukwa inayojengwa na mkandarasi Beijing Construction Engineering company Ltd na kuwataka wananchi wilayani humo kujenga mazoea ya kutunza miundombinu ya barabara kwa kuacha kupitisha mifugo na kuendesha shughuli za kibinadam kando ya barabara ili kuifanya miradi hiyo kudumu kwa muda mrefu.
Hata hivyo miradi iliokaguliwa kupiti ziara hiyo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha ndege katika manispaa ya sumbawanga, barabara ya Ntendo – Kizungu na barabara ya Matai- Kasesya na kumtaka mkandarsi kukamilisha miradi hiyo kwa ubora na kwa muda ulipangwa.
Hata hivyo baadhi ya wananachi mkoani Rukwa wameipongeza serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi hiyo na kwamba itasaidia kuongeza mzunguko wa biashara na kurahisisha usafi na usafirishaji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.