Ofisi ya mkuu wa wilaya ya kalambo mkoani Rukwa imetoa misaada ya vifaa mbalimbli vya ujezi ikiwemo sementi mifuko 2010 na bati bando15 kwenye kata kuminatano za wilaya hiyo ambavyo vitasadia kukarabati majengo chakavu ya shule za msingi na sekondari pamoja na kumalizia maboma ya zahanati na huku ikiwasisitiza watendaji kuvitumia vifaa hivyo kwa malengo yaliokusudiwa.
Kumekwepo na changamoto ya baadhi ya majengo ya taasisi za serikali ikiwemo ya shule za msingi na sekondari kuchakaa na huku baadhi ya maboma kwenye maeneo tofauti ya wilaya hiyo kuto kamilika licha ya nguvu za wananchi kutumika kwa kiasi kikubwa na kupelekea ofis ya mkuu wa wilaya hiyo kuchukua hatua ya kutoa vifaa vya ujezi kwa lengo la kusaidia kuondoa changamoto hizo.
Akikabidhi vifaa hivyo mkuuu wa wilaya hiyo Julieth Binyura kwa viongozi wa kata husika, amewataka wananchi kuendelea kujiunga navikundi mbalimbali vya ujasiliamali ambavyo vitawasaidia kujikwamua na hali ya kiuchumi.
Alisema ziara mbalimbali zilizofanywa ndani ya wilaya ya aliahidi kuchangia shughuli za maendeleo kwa makundi mbalimbali ya jamii na taasisi .
Alisema ametoa misaada katika vijiji vya Mkonko,Namlangwa,Chalaminwe,Safu ,Kisumba ,Sundu,Kilesha, Ilango,Senjakalonje ,Kanyezi ,majengo,Kizombwe,Sopa,Mkowe, Katete.
Katibu tawala wilayani humo Frank Sichalwe amewataka watendaji kusimamia vifaa hivyo kwa umakini ili viweze kutumika katika malengo yaliokusudiwa na kusema jumla ya shilingi milioni tano zimetumika kununua vifaa hivyo.
Mkurugezi mtendaji wa halmashauri ya hiyo Msongera palela aliawataka madiwani kusimamia vifaa hivyo ili viweze kutumika katika malengo yaliokusudiwa na serikali .
‘’kwa ujumla vifaa hivi vimelenga kutatua chanagamoto mbalimbali ambazo sisi kama halmashauri ilitakiwa tuzitatue lakini kupitia hii tuna imani pale ambapo sisi kama halmashauli ilitakiwa tuweke mkono wetu basi misaada hii itaneda kusaidia, lakini namba niwatake watendaji wangu wangu mkasimamie vifaa hivi vizuri.’’alisema Msongera.
Baadhi ya wananchi wilayani humo wameipongeza serikali ya wilaya hiyo kwa kutoa misaada hiyo na kuwa itawasaidia kwa kiasi kikubwa na kuomba kuendelea na moyo huo.
Llicha ya hilo ofis ya mkuu wa wilaya hiyo pia imetia misaada ya vifaa mbalimbali vya ujezi kwa wananchi waliokuwa wamekubwa na maafa ya mvua katika kata ya za lyowa na Matai na hivyo kupelekea nyumba zao kuezuliwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.