Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa huo kusimamia kwa karibu uingizwaji wa pembejeo za kilimo na kuhakikisha zinauzwa kwa bei elekezi ili kuwafikia wakulima kwa muda muafaka.
Akiongea kupitia madhimisho ya ufunguzi wa msimu mpya wa kilimo kwa mwaka 2019/2020 Wilayani Kalambo,Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Julieth Binyura,amesema katika kipindi cha mwaka 2019/2020 mkoa unalenga kulima jumla ya hekta 603,637.5 za mazao mbalimbali.
‘’kati ya hizo hekta 524,800.7 ni za mazao ya chakula ,hekita 76,363.08 za mazao ya biashara na hekta 2,473.35 za mazao mbalimbali ya mbogamboga na matunda. ‘’alisema Binyura .
Alisema jumla ya tani 1,731,495.5 za mazao zinategemewa kuzalishwa ambapo kati ya kiasi hicho tani 1,602,5201.1 ni za mazao ya chakula ,tani 115,800 za mazao ya mbogamboga na matunda.
‘’nitoe maelekezo kwa watendaji wote wa Halmashauri zote kuhakikisha mbolea hizi zinauzwa kwa bei elekezi na zinawafikia wakulima katika maeneo yote’’alisema Binyura.
Mwakilishi wa tasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Briten, Progers Mbugi,amesema mpaka sasa wameweza kufikia wakulima 54,000 kwa kuwapatia elimu na misaada mbalimbali.
‘’mpaka sasa kupitia mradi huu tumeweza kuwafikia zaidi ya wakulima wadogo wadogo 54,000 wake kwa waume ,kutoka katika vyama vya msingi vya ushirika vya mazao –AMCOS pamoja na wale walio nje ya vyama hivi. Lengo letu hadi kufikia mwisho wa mradi huu 2020 tuwe tume wafikia wakulima 72,000.’’Alisema Progers Mbugi.
Kwa upande wa wakulima wilayani humo wameiomba serikali kutoa pembejeo za kilimo mapema kabla ya msimu kuanza.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.