Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kuwa vyuo vikuu vyote nchini vitafunguliwa kuanzia Juni 1, 2020.
Wanafunzi wa kidato cha sita nchini Tanzania ambao wanakaribia kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya sekondari nchini humo pia watarejea shuleni siku hiyo.
Rais Magufuli amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kwa kuwa kasi ya ugonjwa wa corona imepungua nchini Tanzania.
"Hali ya ugonjwa wa Corona nchini imeshuka sana hivyo, sisi kama serikali tumeamua kufungua vyuo vyote Juni 1, 2020 kwahiyo Wizara zinazohusika zijiandae ili vyuo vitakapofunguliwa isitokee kero zingine," ameeleza Magufuli.
Magufuli hata hivyo amesema wanafunzi wengine bado kunahitajika muda wa kufanya tathimini.
"Kwa shule za msingi na madarasa mengine ya sekondari tujipe muda kidogo.tutatathimini maendeleo ya wengine waliofungua kwanza. Hawa wa chuo kikuu ni watu wazima, wanajitambua," amesisitiza rais Magufuli.
Taasisi zote za elimu nchini Tanzania zilifungwa katikati ya mwezi Machi mara baada ya Tanzania kuthibitisha mgonjwa wa kwanza wa virusi vya corona nchini humo.
Pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.John Pombe Magufuli ameruhusu michezo yote ikiwemo Ligi kurejea kuanzia Juni 1,2020 .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.