• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Kalambo District Council
Kalambo District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya sekondari
      • Maji
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo na Ushirika
      • Ufugaji na Uvuvi
    • Vitengo
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
      • Mazingira
      • TEHAMA na Uhusiano
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
      • Kituo Cha Afya Matai
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Upimaji wa Viwanja na Mipango Miji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Uongozi na Mipango
      • Elimu Afya na Maji
      • Ujenzi Uchumi na mazingira
      • UKIMWI
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Mradi unaoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Bajeti ya Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Salary Slip

Rais Magufuli Atekeleza 79% Ya Ahadi Za Barabara Mkoani Rukwa.

Posted on: September 16th, 2019


Mkuu wa mkoa wa Rukwa Mh.Joachim NWangabo amesifu juhudi za Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuhakikisha anatekeleza ahadi zake alizoahidi kipindi cha kampeni baada ya kutembelea barabara zinzoendelea kujengwa katika maenero tofauti ya mkoa huo ikiwemo Kalambo na Nkasi.

Awali akikagua utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya lami katika miji wa Namanyere wilayani Nkasi mkuu  wa mkoa  huo Joachim Wangabo , amesema ahadi ya mheshimiwa rais ni kujenga barabara zenye jumla ya kilometa tano katika mji na mpaka kufikia mwezi Disemba mwaka 2019 zitakuwa zimefikia jumla ya kilometa 3.95 ambayo ni sawa na asilimia 79 ya utekelezaji wa ahadi zake na hivyo kumtaka mkandarasi nayeendelea na ujenzi wa barabara ya kilometa moja afanye haraka kumalizia ujenzi huo ili wananchi waweze kutumia barabara ambazo zimefungwa kwa muda wa mwaka ili kupisha ujenzi.

“Huyu mkandarasi anayejenga kilometa moja kwa kiwango cha lami kazi yake inasuasua kwasababu mradi huu ulipaswa kukamilika mwezi wa sita mwaka huu na sasa ni mwezi wa tisa, kazi haijakamilika lakini pia kuna kero ambazo zipo ndani ya barabara hizi, kuna vivuko vimewekwa vya muda na kwengine hakuna, watu wanapata shida kuvuka mitaro kwenda kufanya biashara zao lakini pia kwenye matolea ya barabara kuna vifusi, hivyo nakupa siku 12 utoe vifusi na ujenge vivuko kwenye mitaro,” Alisisitiza.

Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa barabara hizo ili kutimiza ahadi za Mheshimiwa Rais Mratibu wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijiji Tanzania (TARURA) Mkoa wa Rukwa Mhandisi Boniface William ,alisema kuwa mbali na kujitahidi kuhakikisha barabara hizo zinajengwa kwa wakati lakini kumekuwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti pamoja na upatikanaji wa malighafi za ujenzi wa barabara hizo hasa kokoto.

“katika utekelezaji wa hii miradi kumekuwa na changamoto mbalimbali, changamoto mojawapo ni ufinyu wa bajeti, fedha tunayotengewa kulingana na hali halisi ya ‘site’ unakuta ile fedha ni kidogo kiasi kwamba kama ile barabara ya salala ilikuwa tutengeneze kilometa moja lakini kwa milioni 350 tulishindwa kutengeneza kilometa moja kwahiyo tukaweza kutengeneza mita 700 pekee, tatizo jingine ni malighafi kwa maana ya kuwa na chanzo kimoja cha kokoto katika mkoa, hii inachelewesha kazi,” Alisema.

Katika hatua nyingine, Mh. Wangabo wakati alipomaliza kutrembelea barabara zenye jumla ya kilometa moja katika manispaa ya Sumbawanga amewataka wakandarasi wazawa wanaopewa kazi za ujenzi na TARURA kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia masharti ya mikataba ili kufanya kazi kwa wakati na kuongeza kuwa ikiwa wakandarasi hao hawataonyesha uaminifu katika kazi hizo ndogo itakuwa vigumu kwao kupewa miradi mingine mikubwa.

Katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Nkasi wametengewa bajeti ya shilingi milioni 500 wakati TARURA upande wa Manispaa ya Sumbawanga wametengewa bajeti ya shilingi milioni 460 ili kuendelea kukamilisha ujenzi wa barabara katika kutimiza ahadi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI September 10, 2023
  • Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2023 July 13, 2023
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • Tazama Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA USHAURI YA MKOA WA RUKWA YARIDHIA MAPENDEKEZO YA KULIGAWA JIMBO LA KWELA.

    March 15, 2025
  • RC RUKWA AWAONYA VIONGOZI WANAOKWAMISHA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI SAMAZI

    March 14, 2025
  • WANAWAKE KALAMBO WAFANYA UTALI WA NDANI

    March 10, 2025
  • TALGWU YATOA MSAADA WA KIBINADAMU KWA WANAWAKE WANAOJIFUNGUA

    March 10, 2025
  • Tazama Zaidi

Video

MHE. RAIS SAMIA S. HASSAN AMUAPISHA MAKAMO WA RAIS MTEULE DKT. PHILIP ISDOR MPANGO IKULU CHAMWINO
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Huduma za Afya
  • Ardhi na mipango Miji
  • Kujua Kodi ya Ardhi
  • Kalambodc blog
  • TEHAMA
  • Kalmbodc Twitter
  • Kalambodc Facebook
  • Kalmbodc Instagram
  • TAMISEMI

Viunganishi Linganifu

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wakala wa Manunuzi Serikalini
  • Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
  • Mkoa wa Rukwa
  • Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
  • Manispaa ya Sumbawanga

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Watu waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Matai, Kalambo, Rukwa

    Anuani ya posta: P.o box 03

    Simu ya Mezani: 025-2955212

    Simu ya mkononi: +255 622 858 482

    Email: ded@kalambodc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.