Raisi wa jamhuri ya mungano waTanzania Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia kufanya ziara katika mkoa wa Rukwa kwa muda wa siku tatu kunazia tarehe oktoba 6,2019,Katika ziara hiyo atafungua tarehe 6,2019atazindua mradi wa barabara yaTunduma –Sumbwanga na kuzungumza na wananchi .
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ni kuwa Tarehe7,10,2019 Mh.Rais atazindua mradi wa maji safi na usafi wa mazingira katika Halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga na badae tarehe hiyo hiyo atazindua msikiti wa Istiqaama Community of Tanzania na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa mkoa wa Rukwa.
Tarehe 8/10,2019 Mh.Rais atafungua barabara ya Sumbawanga –Kanazi na ataelekea wilayani Nkasi katika mji wa Namanyere ,ambpo atazindua kituo cha afya Nkomolo-Namanyere kwa niaba ya vituo vya afya vilivyojengwa mkoani hapa na badae atazungumza na wananchi wa mji wa Namanyere.
‘’nitoe Rai kwa wananchi wa mkoa wa Rukwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wetu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ikizingatiwa kuwa Raisi wetu amefanya mambo makubwa ya kuleta maendeleo katika taifa letu na mkoa wetu kwa ujumla.’’Joachim Wangabo mkuu wa mkoa wa Rukwa amesisitiza.
‘’Pia natambua kuwa wananchi wa mkoa wa Rukwa ni wakarimu sana,hivyo ni matumaini yangu kuwa tutampokea kwa hwshima kubwa na kushiriki mkutano mkubwa wa hdhara utakaofanyika katika uwanja wa Mandela .milango ya kuingia uwanjani kwenye mkutano wa hadhara itakuwa wazi kuanzia saa 11:00 Alfajiri mpaka saa 5:00 asubuhi’’Joachim Wangabo mkuu wa mkoa wa Rukwa amesisitiza.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.