Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amewataka mafundi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalmu katika kijiji cha msanzi wilayani Kalambo kuharakishwa ujenzi huo ili kuruhusu wanafunzi kuanza kunufaika na huduma mapema iwezekanavyo.
Ameyasema hayo baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kalambo ikiwemo Bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalmu katika kijiji cha Msanzi ambao ujenzi wake ulianza kutekelezwa rasmi februali 2023 na kusisitiza ujenzi huo kukamilika kabla ya Agost 20 /2023.
Hata hivyo ujenzi wa bweni hilo ulianza baada ya Halmashauri kupokea fedha kutoka serikali kuu, fedha ambazo zilitolewa na Mh.Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassan baada ya kuaharishwa kwa sherehe za uhuru Disemba 2022
Hivi karibuni akiongea baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa bweni hilo Mkurugezni mtendaji wa Halmashauri hiyo Shafi Mpenda, alisema mradi huo utaboresha mazingira bora ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalmu ndani ya wilaya.Hivyo kukamilika kwake kutasaidia watoto wenye mahitaji maalmu na wazazi kutambua kuwa serikali inatoa elimu bila ubaguzi.
Hata hivyo ujenzi wa mradi wa bweni hilo unatekelezwa kwa force Accont kwa gharama ya shilling million 110,000,000/= ukihusisha bweni litakalo kuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kutoka maeneo tofauti.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.