Mkuu wa mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amewagiza wasimamizi wa fedha mkoani humo kuahakikisha vikundi vya kijamii vya utoaji huduma za kifedha vinasajiliwa na kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo ya serikali.
Ameyasema hayo ofisini kwake wakati akizungumza na wasimamizi wa huduma za kifedha kutoka wizara ya fedha na kuitaka jamii kuwa sehemu ya kuwaibua watu wanao endesha huduma za kifedha bila kuzingatia miongozo ya serikali , ikiwemo kuzisajili taasisi husika na kusisitiza wakuu wa wilaya kushirikina na watendaji wa vijiji na kata ili kuwabaini watu hao kisha kuwachukuliwa hatua kali za kisheria.
Aidha, amewataka Watoa huduma za kifedha mkoani humo kuzingatia utolewaji elimu kwa wananchi wanao chukua mikopo ikiwemo kutoa mikataba inayoeleweka na kukubalika kisheria ili kuepusha kujitokeza malalamiko kutoka kwa wakopaji.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.