Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere amezitaka timu za usimamizi wa afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri za wilaya kuhakikisha kila kifo kinachotokea cha mama mjamzito na mtoto mchanga kinachunguzwa kwa kina kwa kuzingatia Matakwa ya Mwongozo wa ufuatiliaji na tathimini ya Vifo vya akina Mama na watoto Wachanga kwa ajili ya Kuchukua Hatua.
Ameyasema hayo, wakati wa kikao cha kujadili vifo vya akinamama vitokanavyo na matatizo ya uzazi na Watoto wachanga, kilicho fanyika ngazi ya Mkoa, katika wilaya ya Kalambo na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya huduma za afya ya uzazi na mtoto ikiwa ni pamoja na kuhimiza watumishi kuzingatia maadili ya kazi, kuhudumia kwa heshima na kutoa huduma kwa wakati na kwa ubora unaostahili.
Aidha amewataka wakurugenzi kuimarisha usimamizi Madhubuti wa mfumo wa rufaa kwa wagonjwa kwa kuhakikisha magari ya kubeba wajawazito yanakuwa tayari kutoa huduma muda wote yanapohitajika.
‘’Tunawajibika kufanya kazi kwa mshikamano na ushirikiano wa karibu kila mmoja kwa nafasi yake. Vifo vya akina mama na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika, havipaswi kabisa kuwepo katika jamii yetu.’’alisema Makongoro.
Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu, Shafi Mpenda ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa kutoa fedha nyingi zilizowezesha kujenga na kukarabati vituo vya kutolea huduma za afya, ambavyo vimewezesha wananchi kupata huduma karibu na maeneo yao.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.