Mkuu wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo amewataka wananchi kujenga mazoea ya kutunza mazingira kwa kuacha kuchoma moto misitu ikiwa ni pamoja na kuto lima kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la kuondokana na adha ya ukame.
Akiongea mara baada ya kutembelea maporomoko ya Kalambo falls yaliyopo mpakani mwa nchi ya Tanzania na Zambia wilayani Kalambo mkoani humo.Wangabo amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuharibu uoto wa asili kwa kuchoma misitu moto bila kujua athari zake.
‘’ niwatake wananchi waache kuchoma misitu hovyo kwani wanaharibu uoto wa asili na ikolojia yake, lakini pia wanaua wanyama na wadudu. Hivyo niwasihi tutunze mazingira ili yatutunze.”Alisema Wangabo.
Alisema wakala wa hifadhi za misitu TFS hawana budi kuhakikisha wana weka miundombinu bora ya maji, umeme na barabara kuelekea eneo la maporomoko ili kuvutia watalii kwa wingi na kuwasihi wananchi kujenga mazoea ya kutembelea vivutio vya ndani.
‘’tunahitaji watu wafanye utalii wa ndani. Wafike hapa kalambo falls ili wajifunze kwa kuona mandhari iliyopo lakini pia tupende vya kwetu na tuvitangaze tusingoje kusimuliwa.” Alisisitiza.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.