Wakulima wa zao la alizeti katika bonde la ziwa Rukwa wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wameiomba serikali kuweka bei elekelezi kwenye mbegu ya zao hilo kutokana na gharama kuwa juu hivi sasa hali inayosababisha baadhi yao kushindwa kulima zao hilo.
Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa mandalizi ya zao hilo kwenye mashamba yao ,wamesema kuwa changamoto kubwa ni ukosefu wa masoko na bei ya mbegu kuwa kubwa kiasi kwamba wanahofu baadhi yao watashindwa hata kulima zao hilo katika msimu huu.
Wamesema serikali haina budi kuweka bei elekezi ya mbegu ya zao hilo kama ilivyo kwa pembeo nyingine za kilimo kwa lengo la kuwasaidia kuinua kipato chao.
"tunaiomba serikali itutafutie masoko ya uhakika kwani kwa huku kwetu bondeni kuzalisha tunazalisha sana alizeti lakini tatizo ni wapi utaipeleka"walisema.
Afisa kilimo wilayani Sumbwanga Joseph Bakuli amesema lengo ni kuwa zao la alizeti kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati ndani ya mkoa hivyo wananchi wanawajibu wa kulima zao hilo na kuondokana na kutegemea zao moja la mahindi.
Naye mkuu wa mkoa wa Rukwa ,Joachim Wangabo, amewataka wananchi kufuata kanuni bora za kilimo kwa kuwashirikisha wataamu lengo likiwa ni kufikia mafanikio.
Hata hivyo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2018/2019 jumla ya hekta 66,872.15 za alizeti zililimwa katika mkoa wa Rukwa na kupatikana tani 61,651.11.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.