...Maafisa wa Mamlaka za Mikoa na Serikali za Mitaa kutoka katika Mikoa na Halmashauri za Mkoa wa Katavi, Rukwa pamoja na wenyeji Kigoma wamehudhuria mafunzo ya utumiaji mfumo mpya (ulioboreshwa) wa kupanga, kubajeti, na kuripoti (PlanRep) katika ukumbi wa NSSF Kigoma. Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI chini ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta za Umma (PS3) kupitia Shirika la misaada la Watu wa Marekani (USAIDS). Mafunzo hayo yanayohusisha Maafisa Mipango, Mweka Hazina, Waganga Wakuu, maafisa TEHAMA pamoja na Makatibu wa Afya imejikita katika kuwajengea uwezo Maafisa hao juu ya mfumo mpya (PlanRep Web Based) ambao utakua unapatikana kupitia kiambaza (browser) katika kompyuta.
Mfumo mpya wa PlanRep (PlanRep Web Based) ni mfumo ambao umefanyiwa maboresho makubwa kwa kuchukua mazuri yaliyopo katika PlanRep ya awali na kuongeza mengine kwa lengo la kuboresha na kurahisisha zoezi la upangaji bajeti katika Halmashauri zetu. PlanRep mpya itasaidia upatikanaji wa taarifa moja ya bajeti husika (kuondoa ufanyaji mabadiliko katika bajeti mara baada ya kutuma kwenda ngazi nyingine) kwa kila ngazi kutokana na kuwepo udhibiti wa kutosha.
Planrep iliyoboreshwa itawezesha uandaaji wa bajeti kuweza kufanyika katika ofisi yoyote ya Serikali Nchini ambayo imeunganishwa na mfumo huu Mfumo wa PlanRep wa awali ambao unatumika hadi sasa unapatikana kwa kila mtumiaji wa mfumo huo kuinstall katika kompyuta ambayo anaitumia kitu ambacho kimekua kikileta changamoto mbalimbali kwa watumia ikiwa ni pamoja na kuwepo na matumizi ya toleo (version) tofauti la mfumo huu kwa watu tofauti hali inayopelekea matatizo ya upatikanaji wa taarifa za mfumo huo pale zinapoamishwa kwenda katika kompyuta nyingine.
Kupitia Matumizi ya Planrep iliyoboreshwa itarahisisha uandaaji na upatikanaji wa bajeti katika Halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na kuziondolea gharama kubwa iliyokua ikitumika katika zoezi la kuandaa bajeti, gharama ambazo zilizotokana na matumizi makubwa ya uchapishaji karatasi, gharama ya safari,na posho za kuwasilisha bajeti katika ngazi ya Mkoa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI, fedha ambazo kwa sasa zitatumika katiaka utekelezaji wa shughuli nyingine za Halmashauri.
Aidha mbali na mafunzo ya Planrep iliyoboreshwa mafunzo ya mfumo mpya wa matumizi ya fedha za Umma katika ngazi ya kituo cha kutolea huduma (FFARS) yalitolewa kwa Maafisa wote. Mfumo huu hasa utasaidia watumishi walio katika ngazi ya vituo vya Afya, Zahanati pamoja na shule za Msingi na Sekondari kuweza kufanya upokeaji na utumiaji wa fedha kwa kufuata taratibu za kifedha bila ya kuwa na taaluma ya Uhasibu.
Mafunzo hayo yalianza tarehe 7 Agosti 2017 kwa kufunguliwa na Mgeni rasmi Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma na kumalizika tarehe 14 Agosti 2017 huku yakiwaacha Maafisa hao wakiwa na ujuzi wa kutosha juu ya matumizi ya mifumo hiyo, ujuzi ambao unatakiwa kufundishwa kwa Maafisa mbalimbali waliobaki katika Halmashauri. Pia mafunzo hayo yametoa fursa kwa Maafisa waliohudhuria kufanya utalii katika Mkoa wa Kigoma.
Mbali na kanda ya Kigoma, Mikoa na Halmashauri zote nchini zimeshiriki mafunzo hayo kupitia kanda mbalimbali ambazo ni kanda ya Morogoro, Mwanza, Mtwara, Dodoma pamoja na kanda ya Mbeya.
Picha ya pamoja, Mgeni rasmi (katikati-waliokaa), Mkurugenzi wa mradi wa PS3 Taifa Dr. Emanuel Malangalila (wapili kushoto-waliokaa), Mwakilishi OR-TAMISEMI Elisa Lwamiago (wapili kushoto waliokaa) Meneja Mradi Mkoa wa Rukwa Bi. Rose Mangilima (kulia waliosimama) pamoja na washiriki Mkoa wa Rukwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.