Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi 583,180,028 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mbuluma Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa itakayo saidia kuwapunguzia wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kufuata masomo katika shule ya Msanzi iliyopo umbali wa km 20.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi wa shule hiyo msimamizi wa mradi huo Emmanuel Simbaulanga alisema shule hiyo ilianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na kufanikiwa kujenga vyumba 4 vya madarasa na kisha serikali kutoa fedha ambazo zitajenga majengo13 ambayo yatajengwa kwa mfumo wa FORCE ACCOUNT.
Amesema miongoni mwa majengo yanayo jengwa ni pamoja na vyumba vya madarasa 8, Jengo la utawala, Jengo la Maabara, Jengo laTehama, Majengo ya vyoo, pamoja na jengo la Incinerator na tenk.
Awali akiongea na wakazi wa kijiji hicho wakati wa ukaguzi wa mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Makongoro Nyerere ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Wilaya hiyo kuharakisha ujenzi wa mradi huo ili kuwezesha wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo ifikapo Januari 2025.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.