WANANCHI kutoka wilaya za Kalambo na Nkasi mkoani Rukwa wameiomba serikali kuongeza vifaa vya kupimia ugonjwa wa ebola pamoja na kutolewa elimu kutokana na wilaya hizo kuwa na mwingiliano mkubwa wa watu kutoka nchi jirani ya Congo na hivyo kuwa na hofu ya kuenezwa ugonjwa huo.
Wakiongea katika nyakati tofauti wananchi hao,walisema serikali haina budi kudhibiti wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ya Congo kutokana na ugonjwa huo kuripotiwa kuwepo nchini humo.
Wakiwa katika mkutano maalumu uliowajumuisha wataalamu wafya ngazi ya jamii na wadau mbalimbali katika wilaya za Nkasi na Kalambo wamedai kuwa mazingira ya ugonjwa huo ni hatarishi sana na hivyo vifaa vya kupimia ugonjwa huo vinatakiwa kwa wingi hasa kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo kati ya Watanzania na Congo.
Lakini pia wizara ya afya imeshauliwa kuwatumia vyema Waganga wa jadi katika vita hii ya ugonjwa wa ebola kwani watu hao wakielimika vya kutosha watatoa msaada mkubwa kwa kuwaelekeza wateja wao kwenda hospitalini pale wanapobaini kuwa wateja wao wanaonesha dalili ya ugonjwa huo
Awali akitoa elimu kwa wananchi kutoka wilaya za Kalambo na Nkasi mwakilishi kutoka wizara ya afya Ashole Mshana ,alisema serikali imeanza kutoa tahadhari kwa wananchi dhidi ya ugonjwa huo na kuwasihi wananchi hususani wanaoishi katika mwambao wa ziwa Tanganyika kuwa makini na wageni wanaoingia kwenye maeneo yao husika .
Mkuu wa wilaya ya kalambo mkoani humo Julieth Binyura alisema lengo la serikali ni kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.
Aidha aliwasihi wataalamu kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kuongeza vifaa vya kupimia ugonjwa huo haswa kwa wananchi wanaoingia kinyemera nchini kupitia njia za panya.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.