Wanachama wa chama cha wafanyakazi wanawake wa serikali za mitaa (TALGWU) mkoani Rukwa wametoa msaada wa kibindamu katika hospitali ya wilaya ya Kalambo kwa wanawake wanaojifungua kama sehemu ya mwendelezo wa maadhimisho ya wanawake duniani ambayo kitaifa yalifanyika Machi 8, 2025.
Mwenyekiti wa kamati ya ushauri wanawake TALGWU mkoani Rukwa Kumbukwa Ndimbwa, alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa tiba hatua iliyo wezesha akina mama wajawazito kujifungua salama na kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Baadhi ya wanawake wamesema uwepo wa hospitali hiyo umewapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wakati wa kutafuta huduma bobezi ambazo awali walikuwa wakizipata katika hospitali ya mkoa iliopo umbali wa km 50 kutoka maeneo yao husika
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.