Ligi ya michezo wa mpira wa miguu uliokuwa ukiendelea kufanyika katika uwanja wa Nelson Mandela manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa imemalizika baada ya timu ya polisi jamii Nkasi kuibuka na ushindi wa magoli mawili baada ya kuishinda timu ya Laela magoli mawili huku timu ya polisi wilaya ya Kalambo ikishika nafasi ya tatu
Kamishina msaidizi wa jeshi la polisi mkoani humo ACP. Zakaria Luba amesema mashindano ya ligi hiyo yalianzia ngazi ya wilaya katika Halmashauri nne za mkoa huo yakiwa na lengo la kuiweka jamii karibu na jeshi la polisi katika kutokomeza matukio ya uhalifu na wahalifu.
Amesema timu ya Nkasi polisi jamii imeshika nafasi ya kwanza na kujinyakulia kitita cha shilingi laki moja na elfu hamsini, jezi na cheti, Laela imepata shilingi laki moja na elfu Hamsini na cheti na timu ya Kalambo Polisi Jamii imejinyakulia fedha kiasi cha shilingi elfu hamsini na cheti.
Kupitia mashindano hayo mkuu wa mkoa wa Rukwa Queen Sendiga amelitaka jeshi la polisi mkoani humo kuifanya michezo hiyo kuwa endelevu na kuwataka vijana kuisaidia serikali katika kukemea vitendo vya ukatili na upotofu wa maadili.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.