Wananchi mkoani Rukwa wameanza siku tatu za maombi ya kumshukuru Mungu baada ya Rais wa jamhuri ya muhangano wa Tanzania John Pombe Magufuli kusema maambukizi ya Covid-19 nchini yamepungua.
Hii inafuatia ushauri wa Rais Magufuli alioutoa alipokuwa wilayani Chato mwishoni mwa juma aliwataka wananchi kutumia siku tatu hizi, kuanzia Ijumaa mpaka Jumapili wiki hii kumshukuru Mungu kwa kuitikia maombi ya kuliepusha taifa na janga la Covid-19.
''Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia'', alisema Rais Magufuli.
Katika kuunga jitihada hizo viongozi wa dini pamoja na wananchi mkoani Rukwa wameanza ibada ya kumshukuru Mungu ili kuwaepusha na janga la corona huku viongozi wa dini wakitoa tahadhari kwa wananchi kuendelea kuwa makini kwa kuzingatia kanuni zinazotolewa na wahudumu wa afya katika kuepukana na ugonjwa huo .
Ambele mwaipopo ambae ni askofu wa KKT Dayosisi ya ziwa Tanganyika, amesema wamekusanyika kumshukuru Mungu kwa kuwanurusu na ugonjwa hatari wa covid 19 ambao umeathiri mataifa mengi duniani.
Amesema wanaimani Mungu anawasikia hivyo kila mtu anawajibu wa kutojisahau na badala yake kuchukua hatua dhidi ya ugonjwa huo ambao umekuwa tishio.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.