Wafanyakazi wakiwemo watumishi wa umma na mashirika binafus mkoani Rukwa wametakiwa kuendelea kumwenzi hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuenzi na kudumisha misingi ya uwajibikaji alio uacha enzi za uhai wake.
Katika kumwenzi hayati baba wa taifa walimu Julius Kambarage Nyerere, Baraza la la wafanyakazi wilayani Kalambo limeketi katika kikao cha pamoja na kusisitiza wafanyakazi kuendeleza misingi ya uwajibikaji alioiacha baba wa taifa enzi za uhai wake.
Dastani Mshanga ambae ni kaimu katibu wa chama cha walimu CWT mkoa wa Rukwa, amesema mwalimu nyerere aliacha misingi mizuri ambayo kila mfanyakazi anapaswa kuitekeleza kwa vitendo.
Raphael Mikoma ambae ni mwenyekiti TUGE wilayani Kalambo,alisema watamkumbuka mwalimu Nyerere kwa kuhamasisha uwajibikaji na uzalendo kwa watanzania na kusema ili kumwezi kila mtumishi anawajibu wa kuyaenzi matendo yake kwa vitendo.
Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi wilayani humo ambae pia ni Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Msongela Palela, alitumia fulsa hiyo kuwasihi na kuwahimiza wafanyakazi kuhamasisha wananchi kujenga nyumba bora za watumishi ili serikali iweze kumalizia sehemu inayobakia.
Baraza la wafanya kazi ni chombo cha kuwashirikisha wafanyakazi katika kuhakikisha kuwa malengo ya halmashauri husika yanafikiwa kama yalivyo kwenye dira,mwelekeo na mpango wa maendeleo wa Halmashauri .
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.