Waathirika 32 wa kimbunga katika kata ya Lyowa na Matai wilayani Kalambo mkoani Rukwa wamepatiwa msaada na serikali ili kurejesha makazi yao ambayo yaliharibiwa na upepo na kusababisha kaya 65 kukosa makazi.
Afisa mipango na uratibu wa halmashauri ya wilaya ya Kalambo Erasto Mwasanga amesema misaada iliyotolewa ni pamoja na mbao 442, bati 400 na misumari kg 103 na kwamba msaada huo umegawanywa kwa waathirika ambao walikumbwa na adha ya nyumba zao kuezuliwa na upepo Septemba 20-2024.
‘’waathirika wanaogawiwa vifaa leo wapo thelathini na mbili kwa mchanganuo ufuatao,kijiji cha namlangwa 7, Matai B 12 na kijiji cha Kateka 13’’Alisema mwasanga
Mapema akigawa vifaa hivyo mkuu wa wilaya hiyo Dkt Lazaro Komba ametoa siku saba kwa mhifadhi wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) wilayani humo kugawa miti kwa wananchi katika maeneo husika ambayo itasaidia kujikinga na adha ya upepo ambao unaweza kujitokeza.
Aidha ameongezea kwa kusema kuwa kila mwananchi ana wajibu wa kupanda miti katika maeneo yao ya makazi na maeneo ya wazi ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba bora na imara kwa lengo la kuepuka athari hizo kujitokeza tena.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.