Wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kupitia jeshi la akiba wilayani kalambo mkoani Rukwa wameonywa kutojihusisha na vitendo viovu pindi watakapo rudi uraiani na kusisitizwa kujikita zaidi katika shughuli za uzalishaji mali na kulinda raia na mali zao.
Mafunzo hayo ya mehusisha wahitimu wapatao 134 kati yao wanaume 99 na wanawake 35 huku wakitakiwa kuwa raia wema na kichocheo cha amani na utulivu wilayani kalambo na taifa kwa ujumla.
Akisoma risala kwa niaba ya wahitimu hao Jen Ngonyani, amesema kupitia mafunzo hayo wamejifunza mbinu mbalimbali za kivita kwa nadhraia na vitendo vikiwemo usomani ramani, utimamu wa mwili, nidhamu na uzalendo huku wakiiomba serikali kuweka utaratibu maalumu utakao wawezesha kupata ajira za kudumu na za muda ili kunufaika kiuchumi.
licha ya hilo, wameiomba serikali kuongeza muda wa mafunzo kwani muda uliowekwa ni mdogo na hivyo kushindwa kujifunza baadhi ya masomo mengi yakiwemo matumizi ya aina nyingi za siraha.
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo wakati wa kufunga mafunzo, katibu tawala wa wilaya Frank Sichalwe akawataka wahitimu hao kuyatumia mafunzo hayo kuwakamata wahalifu wote.
Aidha amewaagiza watendaji wa vijiji na kata kuhakikisha wanashirikiana na askari hao katika kuwabaini waharifu wakiwemo watu wanaolewa wakati wa saa za kazi.
Kwa upande wake mshari wa mgambo wilayani humo meja Gwamaka Mwailunga, amesema mafunzo hayo yalianza julai 13 ,2020 na kuhitimishwa leo julai 17, 2020, mafunzo yaliyodumu kwa muda wa miezi mitano tangu kuanza kwake.
Amesema mafunzo hayo yatakuwa mwarobaini wa kukomesha matukio ya wizi kwa baadhi ya maeneo ambayo asikari hawafiki kwa urahisi na kuwataka wahitimu hao kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kujikita katika shughuli za uzalishaji mali zikiwemo za kilimo.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.