Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imekabidhi vifaa mbalimbali vya kujifunzia na kufundishia katika shule sita za msingi, wanafunzi wenye hali ya ulemavu wapatao 257 kati yao wavulana wakiwa157 na wasichana 100 ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kuyawezesha makundi hayo kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.
Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa inajumla ya shule za msingi 98 kati ya hizo shule 6 ni za makundi maalumu ya walemavu na shule 92 zinazosalia zinaendesha elimu jumuishi.
Akiongea kupitia kikao kilicho jumuisha walimu wakuu pamoja na waratibu wilayani humo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jeshi Lupembe amesema vifaa hivyo ni kwa ajili ya kufundishia, kujifunzia na visaidizi kwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu na kusisistiza walimu kuongeza bidii ya ufundishaji ili kuyawezesha makundi ya wanafunzi wenye ulemavu kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Afisa elimu wa shule za msingi wilayani humo Rose Mganga, alisema vifaa hivyo vilipokelewa kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEM kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa viungo, akili, macho, ngozi na usikivu.
Baadhi ya vifaa vilivyo letwa ni pamoja na vitimwendo 3, lotion maalumu kwa ajili ya wenye ulemavu wa ngozi dazani 3, bembea 1, midori na kengere’’ alisema Mganga .
Hata hivyo shule zilizonufaika na mgao huo ni shule ya msingi Matai A, Kalepula,Myunga , Kale, Mao, Mbuluma, na Kipwa.
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.