MKUU wa mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ameziagiza Halmashauri mkoani humo kuhakikisha zinakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 2888 ili wanafunzi waliokosa nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza waweze kwenda Sekondari.
Agizo hilo alilitoa jana wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri mkoa wa Rukwa(RCC) katika mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi uliopo katika jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa huo.
Alisema kuwa wanafunzi Waliofaulu darasa la saba mwaka 2019 ni 16,069,kati ya hao wavulana ni 7,953 na Wasichana ni 8,116, na nafasi zilizopo ni 13,128.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Wanafunzi ambao watakosa nafasi katika Halmashauri ya wilaya ya Kalambo ni 361,wilaya ya Nkasi Wanafunzi 1554, wilaya ya Sumbawanga Manispaa ni Wanafunzi 179 na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni Wanafunzi 794.
Kutokana na takwimu hizo Halmashauri ya Nkasi inaongoza kwa kuwa na Wanafunzi wengi watakao kosa nafasi ikifuatiwa na Halmashauri ya Sumbawanga, Kalambo na Halmashauri ya Manispaa.
Aidha Wangabo aliwaagiza wakuu wa wilaya za mkoa huo kuhakikisha kuwa wanafunzi wote waliofaulu wanajiunga kidato cha kwanza ifikapo Januari 2020 na kuwa hakutakuwa na udahili wa pili wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2020.
Katika kikao hicho mbunge wa mkoa huo wa Rukwa Silafi Maufi alishauri kuwepo na kawaida ya kuwapima mimba wanafunzi mara kwa mara kuliko kusubilia mpaka ahisiwe mwanafunzi kuwa na ujauzito na wanaume walio sababisha mimba hizo wakamatwe na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo mkoa huo wa Rukwa unajumla ya wanafunzi 294 waliokatisha masomo kutokana na kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka huu wa 2019.
Mwisho
Matai, Kalambo, Rukwa
Anuani ya posta: P.o box 03
Simu ya Mezani: 025-2955212
Simu ya mkononi: +255 622 858 482
Email: ded@kalambodc.go.tz
Copyright ©2018 Kalambo DC . All rights reserved.