Wananchi katika kijiji cha kafukoka kata ya Kisumba wilaya ya kalambo mkoani Rukwa wamelazimika kusimamisha msafara wa naibu waziri wanchi ofis ya RaisTamisem Josephat Kandege nyakati za usiku baada ya tembo kuvamia kijiji hicho kisha kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Kijiji cha kafukoka kinapatikana katikati ya msitu wa hifadhi ya kalambo asilia lakini licha ya hilo kijiji hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto ya tembo kuvamia makazi ya wananchi kila wakati ikiwemo kuharibu mazao na hivyo kupelekea kujitokeza kwa malalamiko kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo na huku wakiomba serikali kutafuta njia mbadara ya kuzuia tembo hao.
Awali wakiongea kwamasikitiko makubwa wananchi kijijini hapo mara baada ya kuzuia msafara huo nyakati za usiku ,walisema walilazimika kuzuia msafara huo baada ya tembo kusababisha kifo cha victor Tanganyika mwenye umri wa miaka 69 mkazi wa kijiji hicho.
Joel Lusambo mkazi wa kijiji hicho , alisema tatizo hilo ni la muda mrefu kwani tembo hao wamekuwa wakivamia makazi yao kila wakati na hivyo kusabisha hofu na mashaka kwenye maisha yao.
Alisema wakati mwingine wamekuwa wakishindwa kwenda hata shamba kwa kuhofia kuuwawa na wanyama hao kutokana na kijiji chao kuzungukwa na msitu wa kalambo asilia.
Janual Mashaka mkazi wa kijiji hicho alisema mzee huyo alikuwa katika shughuli za shamba , ambapo bila kujua hili wa lile alijikuta akivamiwa na tembo huyo na kupelekea umauti kumfika.
Alisema kutoka na hali hiyo ilipelekea waanaanchi kukaa kikao cha dharulaa na kukubaliana kuzuia msafara wa naibu waziri lengo likiwa ni kutaka kujua msimo wa serikali juu ya tembo hao.
Kwa upande wake Naibu waziri wa tamisemi Josephat Kandege, alisema serikali iko pamoja na wananchi na kuwasihi kuendelea kuimani serikali kwani inaendelea kutafuta ufumbuzi zaidi juu ya swala hilo.
Hata hiyo siku za hivi karibuni serikali kupitia wakala wa hifadhi za msitu wilayani humo ilitoa mizinga 100 kwa wananchi wa kata ya kisumba na kusisitiza wananchi kuitumia mizinga hiyo kama njia mbada ya kupambana na tembo kuvamia makazi yao.